October 18, 2018

MSHAMBULIAJI wa Stand United, Alex Kitenge amedai  hali ngumu ya uchumi inayoikumba klabu hiyo inamfanya afikirie kurudi kwao Burundi ili akaangalie maisha mapya ya soka. Mshambuliaji huyo amekiri kwamba Stand inapitia mazingira 
magumu kiuchumi. 

“Ni miezi minne imepita sijapata mshahara wangu  na wala sielewi nitapewa lini, nimejaribu kuongea na uongozi wamesema watanipa mshahara wangu ili niendelee kuitumikia  klabu hii, tofauti  na hapo mimi naondoka kwetu ili nikajipange upya na kuangalia timu nyingine ambayo inaweza kunilipa  kulingana na huduma ninayoipa timu husika,” alisema Kitenge ingawa viongozi wake wamekwepa kuzungumzia hali inayoendelea ndani ya timu hiyo.


Stand  United itacheza na Wekundu wa Msimbazi, Simba Jumapili, Taifa. Stand ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu Bara ambazo zinahaha kikubwa ikielezwa kwamba ni kukosekana kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Bara inayoendelea

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic