October 18, 2018


SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe imeahidi msaada wowote kwa Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kuhakikisha timu hiyo inafuzu Afcon. 
Mwakyembe amesema kuwa; “Nimefurahishwa sana na matokeo haya , vijana wamenikuna uwezo waliouonyesha ni mzuri, sisi kama serikali tutakuwa tayari kumsapoti mwalimu kwa chochote anachokihitaji ili kuweza kufanikisha kucheza Afcon.”

 “Tumefurahishwa lakini tusiwe na miluzi mingi, masuala ya kiufundi tunamuachia mwalimu aweze kufanikisha malengo.

 “Pia nimefurahishwa na muitikio wa mashabiki uwanjani kushangilia, huu ndio uzalendo unaotakiwa, tutumie njia hii kuwamaliza Uganda wakija hapa nyumbani, nawapongeza sana,” alisema Mwakyembe akiizungumzia Stars ambayo ikishinda mechi ijayo dhidi ya Lesotho inafuzu kama Uganda akimpiga Cape Verde.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic