October 17, 2018


Baada ya timu ya Tanzania "Taifa Stars"kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Fainali  za Mataifa ya Afrika (Afcon) ,kambi ya timu ya Taifa imevunjwa kibabe na kuwaruhusu wachezaji kuweza kutumikia timu zao.

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo alisema kuwa wanawashukuru watanzania kwa kujitoa kwa ajili ya timu ya Taifa hivyo waendelee kuwapa sapoti .

"Tumevunja kambi rasmi na kuwaruhusu wachezaji waweze kushiriki katika majukumu yao ndani ya klabu zao kwa kuwa ligi kuu inatarajiwa kuendelea  baada ya kusimama kupisha ratiba za mechi za kimataifa, wachezaji wa kulipwa nao  watarejea kwenye timu zao"alisema



1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic