October 17, 2018


Kocha wa viungo  wa timu ya Simba raia wa Tunisia Adel Zran ambaye yupo makini katika kuhakikisha wachezaji wanakuwa bora kutokana na mazoezi wanayopata amewazuia wachezaji wa Simba kula chips yai.

Zran mwenye elimu ya masuala ya viungo na PhD ya Udaktari wa Sayansi ya Michezo anashughulika pia na kuhakikisha viwango vya wachezaji vinakuwa sawa na kuweza kuzuia majeraha ya mara kwa mara.

"Chips kuku,mayai siyo chakula kizuri kwa wachezaji kwa kuwa mafuta  siyo mazuri sana kwao,mfano wachezaji wangu siku tatu  kabla ya mechi hawawezi kula chips ni marufuku,ila baada ya siku mbili wanaweza kula japo siyo sawa.

"Kabla ya mechi kila kitu kuhusu chakula kinakuwa kwenye mpangilio maalum na isitoshe wachezaji wenyewe wanaelewa kwamba wao wanacheza mpira wa kulipwa sio wa riadha hivyo ni muhimu kuzingatia"alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic