October 3, 2018






Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kipindi kipya chenye mahadhi ya  pranks (kumstua mtu huku ukimrikodi anavyostuka, bila yeye kufahamu), kinaanza mwezi Oktoba.

Katika mahojiano maalum na mwasisi na mendeshaji wa kipondi hicho, mwanahabari wa kimataifa wa Tanzania Joseph Msami, ambaye hivi karibuni alikuwa mtayarishaji wa vipindi wa Idhaa ya Kisahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York, amesema STUKA ni kipindi amabacho kitawaelimisha watanzania kaika Nyanja mbalimbali kama za kijami, kiuchumi kwa kutumia mbinu za burudani.

Msami amesema kipindi hicho ambacho hutumia mbinu ya kamera isiyo hadharani na kuwanasa wakazi katika pitapita zao za kila siku, hakimlengi mtu maalum wala kumuandaa yeyote (Reality Show) na kitatoa burudani ya kutosha kutokana na maadalizi yaliyofanywa na timu ya STUKA kwa zaidi ya miezi mitatu.

Amesema timu hiyo inayojumuisha wataalamu wa maudhui ya habari, picha na sauti imekuwa katika mafunzo maalum yaliyolenga kuhakikisha umma unapata elimu na burudani kwa kuzingatia weledi.

Kipindi chicho kitakachorushwa na kituo cha  televisheni ya TVE katiak muda ambao watazamaji wengi huangakia runinga (Prime Time ), na kurudiwa mara kadhaa ili kutoa fursa kwa watazamaji kuona kwa wingi,

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic