October 2, 2018

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Umande Chama, amelitolea ufafanuzi suala la mchezaji wa Simba, Mghana, James Kotei kumpiga beki wa Yanga, Gadiel Michael.

Chama amesema kuwa tukio hilo ni la kawaida kwenye mpira wa miguu kama mengine ambayo yamekuwa yakitokea kila mara mchezoni.

Mwenyekiti huyo ameeleza kitendo cha Kotei kutokuadhibiwa ndani ya mchezo huo ni kutokana na Mwamuzi Jonesi Rukiyaa kutoliona tukio lenyewe.

Chama amesema yawezekana Rukiyaa hakuwa katika engo nzuri na ndiyo maana ikapelekea akashindwa kutoa maamuzi ambayo wengi walikuwa wanayawazia.

Kutokana na uwepo wa tukio hilo katika mechi hiyo iliyowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga, Chama amesema linapaswa kupitia kwenye kamera za video kabla ya kutoa maamuzi.

Aidha, kiongozi huyo ameeleza kuwa kwa sasa hawezi kuliongelea zaidi na badala yake kamati husika itakaa na kuja na majibu mazuri zaidi kwa baadaye.

13 COMMENTS:

  1. Sawa tu kuna Ngoma alimtwanga khassan kessy hadharani wakati akiwa yanga na mpaka kaondoka yanga hakuchukuliwa hatua.

    ReplyDelete
  2. Ccm imejaa kila sehemu,fanyeni mnavyotaka timu yabebwa kama kitu gani,TFF nao tulitegemea safari hii itakua nafuu kumbe ni walewale,endeleeni mtapata haki yenu,ikiwezekana mfungieni.

    ReplyDelete
  3. Aibu kubwa sana kukataa goli la wazi,mnasingizia off side,mungu atawashushia hukumu hiyo hamtaamin.

    ReplyDelete
  4. Aibu kubwa sana kukataa goli la wazi,mnasingizia off side,mungu atawashushia hukumu hiyo hamtaamin.

    ReplyDelete
  5. Ccm imejaa kila sehemu,fanyeni mnavyotaka timu yabebwa kama kitu gani,TFF nao tulitegemea safari hii itakua nafuu kumbe ni walewale,endeleeni mtapata haki yenu,ikiwezekana mfungieni.

    ReplyDelete
  6. Kitendo cha kelvin hakikuonwa na maamuzi siku ya pili adhabu ikatoka.

    Banda alimpiga Kavila kule Bukoba refa hakuona siku ya pili tamko likatoka.

    Chirwa alimpiga mchezaji Wa Prison pale Chamazi refa hakuona lkn siku ya pili tamko likatoka

    TFF msilale au mpaka MTU apeleke TV bar na kutoa malalamiko

    ReplyDelete
  7. Kitendo cha kelvin hakikuonwa na maamuzi siku ya pili adhabu ikatoka.

    Banda alimpiga Kavila kule Bukoba refa hakuona siku ya pili tamko likatoka.

    Chirwa alimpiga mchezaji Wa Prison pale Chamazi refa hakuona lkn siku ya pili tamko likatoka

    TFF msilale au mpaka MTU apeleke TV bar na kutoa malalamiko

    ReplyDelete
  8. Kitendo cha kelvin hakikuonwa na maamuzi siku ya pili adhabu ikatoka.

    Banda alimpiga Kavila kule Bukoba refa hakuona siku ya pili tamko likatoka.

    Chirwa alimpiga mchezaji Wa Prison pale Chamazi refa hakuona lkn siku ya pili tamko likatoka

    TFF msilale au mpaka MTU apeleke TV bar na kutoa malalamiko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wazinguaji tuuu maana kitu kinaonekana mbona

      Delete
  9. Kitendo cha kelvin hakikuonwa na maamuzi siku ya pili adhabu ikatoka.

    Banda alimpiga Kavila kule Bukoba refa hakuona siku ya pili tamko likatoka.

    Chirwa alimpiga mchezaji Wa Prison pale Chamazi refa hakuona lkn siku ya pili tamko likatoka

    TFF msilale au mpaka MTU apeleke TV bar na kutoa malalamiko

    ReplyDelete
  10. ila shabalala kupigwa kichwa hilo tukio halitapitiwa acheni unazi wenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mzungumzieni na wawa, mnajifanya hamkuliona. Refa aliona akawabeba hakuwa nyekundu. Na refa achunguzwe

      Delete
  11. kibaya wote tunaongea hatuna vyeti vya urefa, sijui wapi tunapata ijasiri kwenye soka letu ambalo kila mtu anajua kuwa hali halisi na mazingir husadifu kilichopo machoni. tatizo ugali umewekwa na aliyeshiba na matokeo yake ni hay.
    tujifunze kufanya kazi kuondokana na ufukara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic