October 2, 2018


Baada ya mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi kuu juzi dhidi ya Yanga, uongozi wa klabu hiyo umemwaga pongezi za dhati kwa kujitokeza kwao.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah, amesema ni jambo jema kuona mashabiki wa Simba wanazidi kujitokeza kwa wingi uwanjani kuendelea kuipa hamasa timu hiyo.

Licha ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Yanga, Abdallah ameeleza kuwa ubingwa msimu huu hauwezi ukaenda popote zaidi ya kuchukuliwa na Simba.

Abdallah anaamini kuwa licha ya Mtibwa Sugar iliyo kileleni hivi sasa mwa msimamo wa ligi haitaweza kusaidia chochote kwakuwa watakata pumzi mapema hivi karibuni.

Kikosi kipana walichonacho Simba kinampa jeuri Abdallah akieleza kikombe cha ligi simu huu lazima kiangukie kwao na kuwanyima tena watani zao wa jadi Yanga ambao walikikosa msimu uliopita.

6 COMMENTS:

  1. YANGA wanapaswa kwenda kumjengea sanamu huyo aliewatengezea tunguli za giza kwenye mechi ya Jana la sivyo wangepigwa kichapo cha aibu jana. Mechi kama ile Simba angefanikiwa kufunga goli moja basi magoli yangeendelea kumiminika misili ya mvua. SIMBA kwa kiwango kile cha jana basi muda si mrefu itakuja kumpiga mtu kipigo cha aibu. Kitu kimoja simba cha kuzingatia timu zote za ligi kuu bara kama zimeambizana jinsi ya mchezo watakaocheza watakapokutana na Simba. Timu zote zimeamua kupaki basi wanapokutana na Simba na kuvizia kaunta attack. Nilijisikia vibaya sana kuwaangalia mashabiki wa Yanga pale uwanja wa Taifa jinsi walivyokuwa na wakati mgumu wakishuhudia timu yao ikicheza kinyonge. Nilitarajia Yanga ingekula sahani moja na Simba kwa kuonesha mchezo wa upinzani lakini cha kushangaza kocha wao anasema waliamua kuwaachia Simba? Kocha wa namana hiyo Yanga hawafai. Simba watarajie kukutana na mchezo wa kupaki basi na kukamiwa na karibu na timu zote labda Azam kwa hivyo inatakiwa kuiandaa timu jinsi ya kupata ushindi kwenye mchezo wa aina hiyo kama wanataka kupata ushindi la sivyo watasumbuka na matokeo ya ajabu.Hakuna anaesema hakuna maombi au uchawi kwani hata uchawi nao ni maombi na maombi ni maombi hata kama unamuomba shetani ila kunakukubiwa na kukataliwa. Hata Warusi wanapozindua kombora jipya au wanaporusha nyambizi hewa zao kuelekea angani basi lazima chombo hicho kipate maombi kutoka kwa wataalam wao wa hadi.Kwa hivyo Simba wanapaswa kuwarusuhusu wazee wa timu kuikagua ile timu au kufanyiwa maombi kwani kizuri chochote ndicho kinachofanyiwa hasada na hata jicho baya la choyo ni uchawi si lazima mtu afukie n'gombe mzima na maisha yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe km nani wa kuipangia Yanga kocha? km unajua mpira sana si uanzishe timu yako ukatafute kocha wa kumuweka?
      Unaandika gazeti kuubwa lkn uchafu mtupu.

      Delete
  2. KUDADEKI MCHAWI KAZIDIWA BASI KELELE TU MITAANI HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAH

    ReplyDelete
  3. Nitaendeleea kusema UCHAWI UKO MIGUUNI MWA WASHAMULIAJI WENU

    ReplyDelete
  4. Ipo hatari simba kufanya vibaya kwenye ligi msimu huu kwa kuamini kuwa wamelogo, basi kila timu mtakayokutana nayo lazma iwaroge.... na wachezaji wenu wakiamini kuwa wanalogwa na mmekwishaa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic