MANARA ANAAMINI ALICHOKIFANYA AJIBU TAIFA ALIPEWA MASHARTI, ASEMA UCHAWI UPO
Na George Mganga
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameamua kufunguka kuhusiana na namna kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajib namna alivyoanzisha mpira kwa kuutoa nje.
Ajib alianzisha mpira huo kwa kuutoa nje baada ya Mwamuzi wa kati, Jonesi Rukiya kupuliza filimbi kuahsiria mwanzo wa dakika 45 za kwanza katika mechi dhidi ya watani zao wa jadi Simba.
Kitendo hicho kimemshangaza zaidi Manara akieleza kuwa hajawai kuona popote pale duniani katika mchezo wa soka kwa mchezaji kuanzisha mpira kwa kuutoa nje.
Manara ameeleza kuwa anajua ni vigezo na masharti ambayo alipewa mchezaji huyo jambo ambalo lilipelekea kuutoa mpira nje badala ya kumuanzishia mwenzake.
"Ibrahim Ajibu Migomba dunia inajua na wewe unajua namna nnavyoikubali miguu yako, na kwangu mim kando ya Kakolanya wewe ndiyo manusura yao leo, maana hapo si bahati mbaya, ni yale masharti na vigezo"
"Nimeangalia mechi za mpira na kwenye TV zaidi ya elfu kumi sijawahi ona hii ya leo, napingana hapa iwekwe kwenye Guinness World Records Book". aliandika.
Aidha, Manara ameeleza kuwa hajawahi kuamini uchawi katika mpira kutokana na timu yake ilivyopata nafasi nyingi dhidi ya watani zao lakini ikashindwa kufunga huku ikiongoza kwa takwimu zote uwanjani.
"Sijawahi kuamini Uchawi katika mpira, lakini huku kwetu upo na unafanya kazi, wameshinda wao 0-0" aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Katika mchezo huo, Simba na Yanga zilienda sulluhu ya kutofungana (0-0) ikiwa ni mechi ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana msimu huu.
Hakuna cha uchawi Manara acha utani. Ajibu kuanza mpira kwa kuuiga nje ni kuashiria fair play. Ila yanga chini ya meneja Nadir Haroub inaweza kuwa yanga ya kihirikina zaidi.
ReplyDeleteHakuna kitu huu ni Mpira, Yanga ilicheza Strategically ndiyo Simba pamoja na kushambulia ili ambulia patupu. Timu bora ni ile iliyozuia mashambulizi na kutokuruhusu goli! Yanga Oyeeee, mtabaki Mikia FC
ReplyDeleteUbora wa timu haupimwi kwa kuzuia mashumbulizi, hupimwa kwa takwimu
DeleteKuna mechi ilikuwa Chelsea sikumbuki na timu gani Denise Wise alikuwa amebet kuwa Chelsea ndio watakuwa wa Kwanza kutoa mpira nje na wao ndio walianza na kweli aliupiga nje bahati mbaya mchezaji wa timu pinzani akauwai. Sikatai mpira wetu mambo hayo yapo na yeye Manara anayajua na ndio maana analalamika kwa kuzidiwa ujanja na Yanga kwa uchawi walioutayarisha
ReplyDeleteKuna mechi kati ya cameroun na guinea bissau pia mpira ulipoanza tu mchezaji wa guinea bissau alipiga nje. Sijaona ajabu yoyote ile
Deletehalafu ukiamini uchawi unawafanya wachezaj wako waamn kuwa jana hawakuwa wazembe kupoteza nafac laumu wachezaji wako wa bilion 2 kwa kushndwa kufurukuta kwa wachezaj wa mil.3 hela si kla k2 yanga wamethbtsha hlo.
ReplyDeletealianza kuthibitisha simbaenzi za manji mlipopigwa 1-0 na pesa zenu
DeleteUnaposema kikosi cha bil.2 ni wivu, kwa kuwa nyie mnatembeza bakuli.
ReplyDeletePili.. Ligi bado mbichi bado mechi 30+ mtaleta mlejesho wa kupaki basi.. Kupata droo kwa simba ndio mnaona ligi imeisha.
Swali la kawaida tu. Hivi baina ya Yanga na Simba baada ya hizi mechi tano nani yuko juu ya mwenzie?
ReplyDeleteKile kitendo cha Ajib kuupiga mpira nje alicheza na akili za kina Haji Manara na ile hofu ikawaingia wachezaji wa Simba na washabiki wao.
Nimeangalia mechi nyingi sana katika uwanja wa mchina zikiwemo za kimataifa na za ligi yetu lakini sijawai kuona na kuwai kufikilia au kuamini kama kuna klabu yoyote ya Tanzania inaweza kucheza mpira uliokwenda shule na wa kiwango cha juu kama walivyocheza simba. Niwe mkweli kiwango kile walichocheza simba sio cha ligi hii bali ni kiwango cha ligi ya mabingwa Africa, simba wamethibitisha kuwa wana kucha wa kiwango cha juu sana. Goli walilokataliwa lilikuwa ni moja ya magori bora kabisa kuwai kufungwa katika ligi za Africa. Wameizidi yanga kila sehemu na wamepiga soka la maana sana sana. Bado kuna mechi zaidi ya 20 kwa kiwango kile hata ubingwa wa Africa unakuja Tanzania kwa mara ya kwanza
ReplyDeletekama Simba wanacheza mpira uliokwenda shule na Simba ndiyo timu bora vipi watoe sare na Ndanda na kufungwa na mbao ???
ReplyDeleteMnashangaa kutoa droo na Yanga na Hamkumbuki kua walishatoa droo na Ndanda na kufungwa na Mbao!!!!!
Kumbukeni kua mechi ijayo itakua baada ya dirisha dogo la usajili na kama hali ya uchumi Yanga itakua nzuri basi Yanga itaongeza nguvu na huenda Simba wakagalagazwa mechi ya pili !
kwa hiyo mbao ni bora kuliko yanga, maana mbao amemfunga Simba, kwa nini yanga hajamfunga Simba iliafanane na mbao,
Deleteau unataka kusema Yanga wanafanana na Ndanda kwa kiwango kwa kuwa yanga ilitoa sare kama waliyotoa ndanda, stupidity arguments
Mimi ni Yanga lakini ukweli lazima usemwe.Simba wamecheza mpira wa hali ya juu sana.Kama timu yao Hai itakaa pamoja muda mrefu basi inaweza kabisa kubadili mwenendo wa soka la vilabu Tanzania.Simba wameshawahi kutufunga lakini jana walituzidi kwa namna ambayo sio rahisi kueleza nä kukubali.Niliomba kwa mara ya kwanza mpira uishe.
ReplyDeletekwani mechi ya Mbao Mwanza mbona Simba ilikosa magoli mengi tu na ikafungwa.Kule kulikuwa hakuna Uchawi? Ni aibu kwa timu kama Simba pale wanapokosa ushindi wanasingizia uchawi vipi mkishinda uwa sio uchawi? Acheni hizo mpira una matokeo matatu
ReplyDeleteMi kwa upande wangu sijaona huo uchawi anaozungumzia Mr Manara.Ila Nimeona uchawi wa washambuliaji wa Simba kushindwa kuona lango na kutikisa nyavu..UCHAWI UKO KWA WASHAMBULIAJI WENU KUKUWA NA PAPARA KILA WAPATAPO NAFASI.
ReplyDeleteMbao na ndanda je? maana nako ulimiliki mpira kwa kiasi kikubwa
ReplyDeleteMbao na ndanda je? maana nako ulimiliki mpira kwa kiasi kikubwa
ReplyDelete