October 1, 2018


Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga SC ulimalizika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya jana.

Kwa sare hiyo, Yanga SC inajisogeza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutokana na kujiongezea pointi moja na kufikisha 13 baada ya kucheza mechi tano, nne nyingine zote wakishinda.

Kwa upande wao, mabingwa watetezi, Simba SC wanafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi sita, wakitoa sare ya pili leo na kufungwa moja, nyingine tatu wakishinda.

Lakini Simba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na pointi zote kwenye mchezo wa leo, kwani walifanikiwa kuwazidi wapinzani wao muda wote.

3 COMMENTS:

  1. Zahera amezungumzia timu yake kushindwa kutumia kaunta attack walizozipata.lakini cha msingi Simba chini ya huyu mzungu inaonekana kuichukua level ya mpira wa Tanzania katika hatua nyengine kabisa ya ubora na inafurahisha. SIMBA hii ikiendelea hivi hivi na kurekebisha madhaifu yao katika safu ya ushambuliaji basi tutarajie makubwa. Kichuya Mohamedi Husein na Erasto nyoni kwanini wasiitwe Taifa Stars? Kuwa na mchezaji kama kichuya ni msaada mkubwa kwa mafowadi kwani baada ya kushuka chini kutafuta mipira kazi hiyo huwa inakuwa na mtu wake wa uhakika tayari. Cha kushangaza wahusika kama vile wanashindwa kufuatilia nyendo za wachezaji wengine wa stars ili kujua nani akicheza na nini kutakuwa na kombanisheni aina gani. Mfano nimefuatilia mechi kadhaa za genki na kugundua Samata anapokuja kucheza Stars huwa anapewaa majukumu tofauti kabisa na ndio chanzo cha Taifa Stars kukosa ushindi. Samata kazi yake ni kufunga magoli pale genk na anafanya hivyo kwa sababu anawapishi wazuri. Samata wa Taifa Stars akahangaike kujitafutia mipira na anapofika golini mabeki washajipanga tayari. Sasa unapowaondoa wapishi wazuri wa mipra kwa mafowadi kama kichuya Taifa Stars sijui kuna maana gani. Samata wa Taifa Stars lazima azungukwe na walshaji wazuri wa mipira kwani Samata huyu si kwakuwa kapteni basi afanye kila kitu uwanjani.

    ReplyDelete
  2. huyu kocha wa yanga naona anafaa zaidi kuwa msemaji wa timu kuliko hii nafasi aliyokuwa nayo, anaongea vitu vya kuwafuraisha washabiki baada ya kuelezea hali halisi ya mchezo...huwezi sema wachezaji uliwafundisha vile alafu baadae unatuambia kaseke na ajib walishindwa kusikiliza kile alichowaelekeza na ndiyo mana aliwatoa baadae sasa hapo sijui tumuelewe lipi labda.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na wewe Nyoni na Shabalala wanafaa kuitwa timu ya Taifa lakini kichuya anastahili kuachwa kama umefatilia mechi za Simba za hivi karibuni yeye amekuwa chanzo cha Simba kushindwa kuondoka na ushindi kwani anakosa nafasi za wazi kama aliyokosa jana pili amekuwa na papara ya kutaka kufunga badala ya kuchezesha timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic