MASHABIKI YANGA WAMPIGIA KELELE PAUL MAKONDA
Mashabiki wa Yanga jana Jumapili walikuwa moto baada ya kumpigia kelele Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na kuvaa jezi ya Simba.
Tukio hilo lilijiri jana Jumapili wakati Simba ikijiandaa kucheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makonda ambaye alitua uwanjani hapo kwenda kupata burudani ya soka, aliingia na kuwasalimia mashabiki wote kwa kuwanyooshea mkono kisha akaenda kukaa VIP.
Lakini wakati akitoa salamu hizo, mashabiki wa Simba walionekana kumshangilia kwa nguvu kubwa lakini wale wa Yanga walimpigia kelele nyingi kama za kumzomea hivi baada ya kuona amevalia uzi wa Simba.
Hata hivyo kiongozi huyo hakuonekana kujali sana kwa kuwa anafahamu mambo ya ushabiki.
Mwigulu nchemba alikuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi hivyo Yanga waliwahi kumpigia kelele?
ReplyDelete