MASHABIKI YANGA WAJIBU MAPIGO SIMBA, WAMVAA MANARA
Mashabiki wa Simba jana waliendelea na mbwembwe zao kwenye mechi dhidi ya Yanga baada ya kuingia na jeneza lenye bendera za watani zao hao ambao nao walijibu mapigo.
Simba na Yanga zilipepetana jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa kwanza kwao msimu huu.
Jeneza hilo liliwashuhudiwa ambapo mashabiki hao wa Simba wakiwa ndani ya uzi mweupe na mwekundu wakiwa wamelibeba huku wakishangiliwa na wenzao.
Lakini baadaye kidogo, Yanga nao walijibu mapigo baada ya mashabiki wao kuingia na jeneza lililovalishwa bendera zenye rangi nyekundu na nyeupe ambazo hutumiwa na Simba.
Siyo mara ya kwanza kwa timu hizi mashabiki wake kufanya vituko uwanjani.
balaaa kwenye soKa la kiweusi..
ReplyDelete