MBOSSO: SIPENDI KUSHINDANISHWA NA ASLAY – VIDEO
Mwanamuziki kutoka Lebo ya WCB , Mbosso Kirungi amesema moja kati ya vitu ambavyo huwa hapendi kuvisikia kabisa ni pale ambapo watu wanamshindanisha na Mwanamuziki mwenzake waliyekuwa naye kwenye Kundi la Yamoto Band kabla halijavunjika, Aslay Isihaka.
Mbosso amesema Aslay ni msanii mkubwa ikilinganishwa na yeye na anamheshimu sana kwani alianza kufanya kazi hiyo ya muziki kitambo na baadaye wakaungana na kuunda ‘Yamoto Band’.
“Moja na vitu ambavyo sipendi kuvisikia ni kushindanishwa na Aslay, huyu ni mwanamuziki mkubwa sana, ameanza kuimba kama Solo Artist mwaka 2012, mimi nimeanza Januari mwaka huu, kwa maana hiyo nina miezi tisa tu. Kunilinganisha naye ni sawa na kumvunjia heshima, ninamheshimu sana Aslay, ni kaka yangu,” alisema Mbosso.
0 COMMENTS:
Post a Comment