October 3, 2018


Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (2018/19), unaambiwa jina la kiungo wa Simba, Shiza Kichuya, limekuwa gumzo kwa wadau wengi na baadhi ya mashabiki wa Simba.

Kichuya mpaka sasa hajafunga bao lolote katika kikosi cha Simba licha ya kufanya vema zaidi msimu uliopita akiwa na timu hiyo.

Kiungo huyo aliyesajilikuwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, amekuwa na mwanzo ambao si mzuri kwa msimu huu jambo ambalo limepelekea kuzua maswali kwa mashabiki na wadau wa timu hiyo.

Katika mechi zote ambazo Kichuya ameshacheza, ameonekana kutokuwa fiti kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi ambazo amezipata akiwa mchezoni.

Moja kati ya mchezo ambao Kichuya alipata nafasi nyingi zaidi na alisjindwa kuzitumia ni katika mechi ya dhidi ya Mbao FC iliyopigwa jijini Mwanza dhidi ya Mbao FC.

Kichuya alionekana kukosa utulivu na kushindwa kutumia nafasi nyingi haswa mipira ya FAULO ambayo mara nyingi alikuwa anapiga nje ya eneo husika.

Kutokana na mwanzo wake kuwa mbaya, mashabiki wengi wamekuwa wakihoji pengina mfumo wa Kocha Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems umechangia.

Wapo waliosema kuwa kikosi kina baadhi ya wachezaji wengine wapya kitu ambacho kitahiji muda kwake ili kuendana na mfumo.

6 COMMENTS:

  1. Hata kulenga lango nako ni kwa sababu ya mfumo au wachezaji wap? Hapana... Kichuya kiwango chake sio kama kile cha zamani, inabdi afanye sana mazoezi ili arudi kule aliko kuwa. Labda ameridhika sasa maana kwa hela amepata kwa kweliii. Wana saikolojia inabidi wakae nae wamuweke sawa.

    ReplyDelete
  2. Hahaahaaa labda amepigwa misumari

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Nafikiri ujio wa Dilunga na Chama umempoteza uelekeo.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli Kichuya sasa hivi amekosa utulivu. Sio Kichuya yule wa misimu miwioli iliyopita. Anahitaji kukaa na wataalamu wa saikolojia wamuweke sawa. Iwapo Dilunga ambaye kwa sasa ni majeruhi atarejea uwanjani huenda akampoteza kabisa Kichuya (kama hata-improve)

    ReplyDelete
  6. hata uweza unaisha asipomsikiza kocha anachosema atapotea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic