October 3, 2018


Licha ya kwenda suluhu tasa ya bila kufungana na Simba Jumapili ya wiki jana, uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa wachezaji wake walicheza mpira kutokana na mbinu waliyoelekezwa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Matawi Yanga, Bakili Makele, amesema kuwa wachezaji wao walifuata maelekezo ya Zahera hivyo hakuna wa kutupiwa lawama kuwa alicheza tofauti na maagizo ya Kocha.

Makele amefunguka na kusema licha ya kutaniwa kuwa wao ni ombaomba na wala mihogo Morogoro, walijitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuwazuia Simba ili wasiweze kufungwa.

Katika mchezo huo Yanga walishambuliwa kwa asilimia kubwa na kipa wao, Beno Kakolanya akionekana kuwa kizingiti kikubwa kwa Simba kwa kuwazuia kucheka na nyavu kwa dakika zote za mchezo.

Wakati huo tayari kikosi cha Yanga kimeshaanza kujifua kuelekea mechi yake ijayo dhidi ya Mbao itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


3 COMMENTS:

  1. Masikini yanga suluhu na Simba wansichukulia ushindi mkubwa kwao kwani kutokana na kuwango chao dhaifu jwa mchezo wote, walitarajia kuchapwa kichapo cha mbwa koko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulishindwaje kumchapa Kama timu yako ilikuwa na uwezo?

      Delete
  2. Yanga haijapoteza mchezo na bado wana mechi moka mkononi... Kwa hivyo matokeo yale ya suluhu ni mazuri kwao. Simba wana pressure na matokeo ya ushindi yalikuwa lazima kwao kwenye ile mechi, kwa kutambua hilo kocha wa Yanga alipanga kikosi chenye uwezo wa kuhimili pressure ya Simba (Au kwa kichina Tai Chi - tumia nguvu za mpinzani wako kummaliza) huku akiwaachia wao wacheze mchezo na yeye ashambulie kwa kaunta, ukweli ni kuwa aliweza kuhimili pressure ya Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic