Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewji, amesema anaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo unaonendelea katika eneo la Bunju jijini Dar es salaam.
Ujenzi huo ambao ni sehemu ya ahadi yake wakati anaomba zabuni ya kuwekeza kwenye klabu hiyo, umefikia hatua nzuri baada ya eneo la kuchezea, kumaliza kusawazishwa na huenda hatua inayofuata ikawa ni kutandika nyasi.
''Tumefika hatua nzuri ya maendeleo ya uwanja wetu wa mazoezi wa Simba. Nafurahi kuona maono yangu yanakamilika ili hata siku nisipokuwepo duniani, uwanja uendelee kutumika kwa mazoezi Insha'Allah'', ameandika Mo Dewji kwenye ukurasa wake wa 'Twitter'.
Mo Dewji alishinda zabuni hiyo ya uwekezaji na kupewa asilimia 49 ya hisa za klabu hiyo huku asilimia 51 zikibaki kwa wanachama wengine. Katika ahadi yake alibainisha kuwa baada ya klabu kupata uwanja wa mazoezi kinachofuata ni kuhakikisha timu inapata mabweni ya kisasa kwaajili ya kambi pamoja na timu za vijana kupata sehemu ya kukaa na kufanya mazoezi ya kila siku.
Tumefika hatua nzuri ya maendeleo ya uwanja wetu wa mazoezi wa #SIMBA. Nafurahi kuona maono yangu yanakamilika ili hata siku nisipokuwepo duniani, uwanja uendelee kutumika kwa mazoezi Insha'Allah.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeletemo ukisema maneno kama hayo unawaumiza wana yanga furaha kwa wanasimba.
ReplyDeleteInaonesha jinsi gani Mo alivyodhamiria kuondoa tatizo la uwanja kwenye team yake hongera sana.
ReplyDelete