VIDEO: KOSAKOSA ZA SIMBA DHIDI YA YANGA HIZI HAPA (FULL HIGHLIGHTS)
Watani wa Jadi wa Tanzania Simba na Yanga jana wameshindwa kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa na burudani kamili ya soka, Simba walitawala zaidi mchezo huku wakitengeneza nafasi nyingi za mabao zilizoishia kuwa kosakosa kupitia kwa washambuliaji wake Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya, kiungo Clautos Chama na beki Shomari Kapombe.
Hata hivyo kunako dakika ya 28 ya mchezo, Simba walifanikiwa kutumbukiza mpira kimiani lakini haikuwa goli bada ya mwamuzi msaidi Frednarnd Chacha kuamua kuwa ilikuwa ni off-side.
Golikipa wa Yanga Bono Kakolanya aliibuka shujaa kwa kuokoa michomo zaidi ya sita kutoka kwa Simba na kuihakikishia timu yake usalama kwa dakika zote 90.
Matokeo hayo yameifanya Yanga ifikishe pointi 13 na kupanda hadi nafasi ya pili kutoka nafasi ya nne nyuma ya vinara Mbao FC huku Simba wakisalia kwenye nafasi yao ya tano na pointi zao 11.
Tazama highlights za mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment