KANGI LUGOLA AINGILIA KICHAPO CHA STARS DHIDI YA LESOTHO, AJA NA MBINU MBADALA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameibuka na kuzungumzia kipigo walichokipata Taifa Stars dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu kuelekea AFCON mwakani.
Lugola ambaye ni mdau wa michezo, amesema matokeo ya kufungwa bao 1-0 na Lesotho yamewasikitisha wengi, jambo ambalo limesababisha kila mtu kuja na kauli yake.
Waziri amefunguka kuwa ni aibu kwa Stars kupoteza licha ya kupewa shilingi za kitanzania milioni na Rais John Pombe Magufuli kama motisha lakini mwisho wake timu ikafungwa.
Lugola ameamua kuja na mbinu mbadala ya kuwataka wadau na mashabiki wa Stars kupiga dua na sala akiamini ndiyo njia pekee ya kuisaidia timu ifanye vizuri.
Dua na sala hizo Lugola anaamini zitafika kwa Mwenyezi Mungu ili kuipa suluhuhisho Stars iweze kufanya vizuri katika mechi ijayo dhidi ya Uganda itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
"Kama imekuwa ngumu kushinda inabidi sasa watanzania wafanye maombi ya duala na sala ili kuiwezesha kupata matokeo, na haswa kuelekea mechi ijayo na Uganda" alisema.
Stars itarudiana na Uganda jijini Dar es Salaam Machi 13 2019 ambapo kama ikishinda itakuwa imefuzu kushiriki AFCON.
Kufuzu kwa Stars itategemeana pia na matokeo ya mchezo kati ya Cape Verde ambao wanapaswa kushinda dhidi ya Lesotho ama mechi iende sare na Stars wakishinda na Uganda watakuwa wamefuzu.
Sawa mheshimiwa lakini kocha wetu ni mbishi sana, sasa sijui nae tumuombee dua.
ReplyDeleteTatizo ni kocha...AMUNIKE OUT
ReplyDeleteHehee kama Amunike angekuwa anajua kiswahili basi naamini mida hii angeshakuwa yuko kwao Nigeria.
ReplyDeleteMheshimiwa, hiyo inaweza ikasaidia, maana hata mimi naona kuwa hapa kitakachosaidia kwenye mechi na Uganda ni SALA na DUA, kwani hivi ndivyo vitakuwa ni muhimu na vyenye ubora kuliko uwezo wa mbinu za Amunike. Hapa naamini kuwa (SALA na DUA > MBINU ZA AMUNIKE).
ReplyDeleteKula nkisikia jina AMUNIKE napata kichefuchefu
ReplyDelete