November 22, 2018


Baada ya Taifa Stars kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Lesotho Jumapili ya wiki iliyopita, Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Mwalimu Alex Kashasha, amemvaa Kocha Emmanuel Amunike juu ya kikosi alichokipinga siku ya mchezo.

Kashasha ameibuka na kueleza kuwa Amunike amekuwa mbishi wa kushauriwa jambo ambalo limepelekea kikosi alichokipanga kiweze kupoteza mechi hiyo.

Mwalimu huyo amesema Amunike amekuwa hakubali kushauriwa hata na wachezaji waandamizi kitu ambacho kinachangia kwa namna moja amana nyingine Stars kuboronga.

Kutokana na kipigo hicho dhidi ya Lesotho, Kashasha amesema wachezaji walikuwa na wakati mgumu mno baada ya mchezo kuisha ambapo walilazimika kulia ndani ya basi sababu ni machungu ya kupoteza.

Mbali na kulia, wachezaji hao waligoma hata kuzungumzia namna mchezo ulivyokuwa kwa namna ambavyo matokeo hayo walivyoyapokea na kwa kuwaumiza.

5 COMMENTS:

  1. AMUNIKE AACHIE NGAZI AWAJIBIKE KWA MATOKEO MABAYA. HUO NDIO UONGOZI WA KUTAMBUA RESPONSIBILITIES.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwwli tutafute kocha wa muda kwanza

      Delete
  2. Sijawahi kuona kocha mwenye msimamo wa kipumbavu kama huyu,unajifanya msomi unaejua soka la bongo na Afrika kumbe hovyo tu,na kama umetumwa kaa ukijua hapa hupawezi utang'oka tu

    ReplyDelete
  3. Kidau na TFF waligoma kutoa wasifu wa kocha Amunike.Walikutana mitaani Lagos na kufanya deal wanayoijua wenyewe kutuletea madudu halafu bosi Karia anasema tusimjadili ?

    ReplyDelete
  4. Benchi la Ufundi siwezi kulitupia lawama, bali naitupia kwa mtu mmoja tu ambaye ni Kocha tu. Nakubaliana na Kashasha kwamba Amunike ni Mbishi na hashauriki. Naliamini hilo, maana hata siku ya mechi na Lesotho, dakika za mwanzo tu wastani kama ilikuwa dkk kati ya 20 hadi 30, baada ya mapungufu kuanza kuonekana, niliona baadhi ya wahusika kwenye benchi la ufundi walikuwa wakimshauri kitu Amunike, lakini kwa mtazamo wa sura yake alionekana kutokubaliana na alichokuwa akishauriwa na akasimama kwa hasira kwenye benchi na kwenda kusimama kwenye Zonal yake ya maelekezo. NAUNGA MKONO KUWA KOCHA HUYU HASHAURIKI na pia ninahiari ya kukubaliana na neno kuwa ni MBISHI. Aende zake tu, miezi minne iliyobaki kabla ya mechi na Uganda, tutakuwa tumepata kocha mzuri, hizo gharama za kumtunza Amunike hadi mwezi wa tatu ni bora avunjiwe mkataba na pia zitumike kumpata kocha mpya au wa muda tu na kuiita Stars mapema ili kocha atakayepatikana awaelewe vijana mapema.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic