July 7, 2018


Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Masoud Djuma, amefunguka kwa kueleza kuwa ana uhakika wa kuwatwanga AS Ports katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya KAGAME.

Djuma ambaye ameshikilia kiti cha aliyekuwa Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeondoka nchini baada ya mkataba wake na Simba kumalizika, amesema anawafahamu vizuri wapinzani wake na watajipanga kuwafunga.

Kocha huyo ambaye ameonesha dhamira ya kuipa ubingwa Simba ameeleza watahakikisha wanapata alama 3 mbele wa ya wadjibout hao ili kuweza kusonga mbele mpaka hatua inayofuata.

Jeuri ya Djuma kuongea kauli hiyo inatokana ushindi wa mechi mbili dhidi ya Dakadaha ya Somalia na APR ya Rwanda huku akienda sare dhidi ya Singida United ya Singida wakati Simba ikiwa kileleni katika kundi C.

Mechi ya Simba dhidi ya AS Ports itapigwa siku ya kesho Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV