November 22, 2018


Na George Mganga

Mchambuzi wa maarufu wa soka kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mwalimu Alex Kashasha, amesema kwa namna mwenendo wa Taifa Stars unavyoenda hivi sasa unaweza ukaipoteza timu.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Kashasha amesema hayo kufuatia kitendo cha Kocha Emmanuel Amunike kupanga kikosi ambacho hakikuwa na nguvu ya kuisiaidia timu kuibuka na ushindi dhidi ya Lesotho kwenye harakati za kuwania kushiriki AFCON mwakani huko Cameroon.

Mchambuzi huyo amepinga mbinu alizokuja nazo Amunike akimuelezea kuwa alikosea kupanga aina ya kikosi kilichocheza na kuwaacha waliokuwa mhimili wa timu.

Kikosi kilichocheza dhidi ya Lesotho na hatimaye Taifa Stars kufungwa bao 1-0, amekipinga akiamini hakikustahili na akiamini ilikuwa sababu kubwa ya vijana kuzidiwa na kuepelekea kupoteza mchezo huo.

Aidha, Kashasha amewashauri viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubali kwanza kuwa kuna mapungufu mengi ndani ya timu ya taifa huku akiwataka lazima wayarekebishe.

Kashasha ameeleza endapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote ama TFF kuingilia kati timu hiyo, basi itaweza kupotea kabisa na kuirudisha nyuma zaidi ikiwezekana itaendelea kufanya vibaya zaidi na zaidi.


2 COMMENTS:

  1. ETI TFF BOSI WAO ANAMKINGIA KIFUA KOCHA ASIJADILIWE HUYU NI WA AINA GANI KIONGOZI UNAYEZUIA TUSIMJADILI NA KUMKOSOA KOCHA WA TIMU YETU YA TAIFA? UONGOZI NI DHAMANA NA WENYEWE WENYE TIMU YAO NI SISI WANANCHI WA TANZANIA. HATUPO GHANA WALA SOMALIA. HII NI TANZANIA TUNA AMANI TUNA DEMOKRASIA.

    ReplyDelete
  2. Kwakwel mwl kashasha ninekupata saana amunike mbinu zake sio za ushindi ni za kuzuia idadi ya magol ya kufungwa tu au ktoa sale yaan timu inakua na "walinzi 9, alaf wafungaji wawil" kwakwel amunike AKABEBE KOROSHO

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic