November 3, 2018


Na Lunyamadzo Mlyuka

Kiungo mkabaji wa timu ya Simba ambaye ni kipenzi cha wanasimba, Jonas Mkude, amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu kwani wamejiandaa kiasi cha kutosha kwa mchezo wao wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mkude amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kuweza kupata ushindi kutokana na maandalizi ambayo wameyapata pamoja na uzoefu walionao kwenye ligi.

"Tupo vizuri kwa ajili ya mchezo wetu tumejipanga kiasi cha kutosha hivyo mashabiki wasiwe na mashaka juu ya hilo watupe sapoti ili tufanye vizuri.

"Ushindani ni mkubwa kwa kuwa timu ambayo inashiriki ligi hiyo siyo ya kuibeza kama ambavyo unajua kila timu inahitaji pointi tatu, hata sisi tunazihitaji pia, tutafanya juhudi kuzipata," alisema.

Kwa msimu huu inakuwa mara ya kwanza kwa Simba kucheza na JKT Tanzania ambayo imepanda daraja msimu huu kushiriki ligi kuu ikiwa chini ya Bakari Shime.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic