November 3, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Singida United Hemed Morroco amesema kuwa kinachoikwamisha timu yake kupata matokeo ni suala la muda kutokana na wachezaji kutokuwa na pacha inayoelewana ndani ya uwanja.


Morroco amesema kuwa amekaa na wachezaji wake na kuzungumza nao kuhusu suala la kupata matokeo uwanjani kutokana na kushindwa kuwa na muunganiko mzuri.


"Bado suala la ugeni linawasumbua, wachezaji wangu hwajazoeana hasa kwa namna ya kucheza ila hilo tayari nimelifanyia kazi hivyo tutaanza kupata matokeo katika mechi zetu zijazo.


"Taratibu watakuwa sawa maana mechi za mwanzo inakuwa ngumu katika kutengeneza pacha ambayo inaweza kupata matokeo ila tunazidi kujifunza na kurekebisha makosa ili kufanya vizuri zaidi kwenye ligi," alisema.


Singida United wamecheza michezo 12 kwenye ligi na wamekusanya pointi 17 ambazo zinawafanya wawe nafasi ya 9 wana kibarua kesho cha kucheza ugenini dhidi ya Alliance ambayo inajikongoja nafasi ya 20 ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza michezo 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic