WAKATI UCHAGUZI SIMBA UKISUBIRIWA KESHO, MWANACHAMA HUYU ATINGA TAKUKURU
Wakati uchaguzi wa Simba ukisubiriwa kwa hamu kesho ili kupata viongozi watakaoiongoza klabu hiyo kwa muda wa mwaka minne, Mwanachama anayejulikana kwa jina la Said Bedui, ameamua kutinga katika Ofisi za TAKUKURU.
Mwanachama huyo amesema ameamua kukimbilia ofisini hapo ili kusaka haki yake ya kutupiliwa mbali kwa rufaa yake aliyopeleka kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Bedui aliwasilisha rufaa hiyo TFF akiomba isikilizwe baada ya kukataliwa na klabu yake ya Simba ikieleza mapingamizi yake hayakuwa na mashiko.
Mapingamizi ya Bedui yaliyokuwa yanahusiana na kuhoji suala la mapato na matumizi yalitupiliwa mbali na Simba ambayo alihitaji yafikishwe kwenye mkutano mkuu.
Baada ya Simba kuyaweka pembeni na kisha kukimbilia TFF, Bedui ameeleza kufika TAKUKURU akiamini kuna suala la rushwa limetendeka hivyo ana imani atapata msaada wa kusaidiwa.








0 COMMENTS:
Post a Comment