Beki wa Azam FC, Abdallah Kheri “Ssebo” amekwenda kufanyiwa uchunguzi wa goti lake.
Beki huyo ni kati ya wale wanaokipiga katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Ssebo aliumia katika mechi ya kirafiki wakati Azam FC ikijipima nguvu.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema tayari beki huyo yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu.
“Wataalamu watamfanyia uchunguzi kwanza ili kujua ukubwa wa maumivu yake,” alisema.
“Baada ya hapo, tutajua hasa nini kifanyika. Kama apate matibabu ya upasuaji au vinginevyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment