Kikosi cha Mtibwa Sugar
imelazimika kubaki Dar hadi itakapokwenda nchini Uganda Desemba 13 kuikabili
timu ya KCC katika mchezo wa kombe la shirikisho baada ya kupata faili la wapinzani wao.
Mtibwa ambayo
inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ilifanikiwa kuitoa timu ya Northern
Dynamo ya Shelisheli kwa mabao 5-0
hivyo imeigia hatua ya pili ya michuano hiyo na itavaana na KCC ya
Uganda.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,
Thobias Kifaru amesema, wamelazimika kubaki Dar kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo wao dhidi ya KCC katika mechi itakayochezwa Desemba 15 ikiwa ni pamoja na kuwasoma wapinzani wao hao.
“Timu imerejea nchini
Desemba sita ikitokea Shelisheli na imebaki Dar ikiendelea na maandalizi ya
mchezo wetu unaofuata dhidi ya KCC hadi kikosi kitakapoondoka jijini kuelekea
Uganda Desemba 13.
"Wachezaji wote wapo vizuri na wanamorali ya hali ya juu
kuelekea mchezo huo baada ya ushindi wa hatua ya awali," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment