December 30, 2018


BAADA ya uongozi wa KMC kuamua kuachana naye kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, mchezaji Abdulhalim Humud amepania kuipandisha timu yake mpya ya Arusha United.

Humud Kwa sasa anaichezea timu ya Arusha United ambayo kocha Mkuu ni Felix Minziro na ndiye aliyeipandisha KMC Ligi Kuu msimu uliopita naye pia aliachwa nafasi yake ikachukuliwa na Ettiene Ndayiragije.

Humud amesema kikubwa anachofurahia ni kuwa na amani ndani ya moyo hivyo ana uhakika wa kufanya makubwa akiwa na timu yake mpya ya Arusha United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

"Kila kitu kinawezekana na maisha ya mpira ni popote hivyo kwa sasa hesabu zangu ni kusaidiana na wachezaji wenzangu kufikia malengo ya timu ambayo ni kuipandisha daraja kutoka hapa ilipo.

"Yale yaliyopita nasahau yote na ndio maana nafanya sana mazoezi kujiweka sawa na kuwa kwenye ubora ule ambao wengi wanautambua, mashabiki watupe sapoti," alisema.  

1 COMMENTS:

  1. Pole sana kama walikusingizia kuambiwa unawachukulia wachezaji wenzio wake zao. Uaminifu ni jambo muhimu sana katika maisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic