December 30, 2018



LICHA ya Mashujaa FC kuwa nafasi ya Saba Ligi Daraja la Kwanza wakiwa kundi B baada ya kukusanya pointi saba katika michezo saba na kushinda michezo miwili na sare mchezo mmoja na kupoteza michezo minne bado hawana hofu na vigogo wa Ligi Kuu.

Katibu wa Mashujaa FC ya mkoani Kigoma, Khatibu Mtumwa amesema wanaona fahari kufanikiwa kuifunga Simba kwenye kombe la shirikisho ni jambo kubwa ambalo limewapa furaha hivyo wana uhakika wa kupanda daraja msimu ujao.

" Morali kwa wachezaji imekuwa kubwa kwa sasa na kocha amewapa mbinu mpya ambazo zinawafanya wazidi kujiamini hivyo tuna uhakika kuanzia sasa tutakuwa na balaa kwa kila mchezo.

"Hesabu zetu kwa sasa ni kumyoosha kila tutakayekutana naye kwenye Ligi ili tuweze kupanda na kucheza nao huko huko waliko hao wanaoitwa Azam, Yanga ili tuthibitishe ubora wetu," alisema.

1 COMMENTS:

  1. JEURI YOTE HII NI MAKOSA MAKUBWA WALIYOENDELEA KUIFANYA SIMBA YA KUDHARAU MECHI. MASHUJAA WATAMBUE YANGA SIO SIMBA. YANGA ITAWABAMIZA VIZURI HAWADHARAU MECHI. WASIJIONE SASA WANA UBAVU WA KUZIFUNGA TIMU ZOTE KUBWA. WAJE NA HESHIMA KWA YANGA WASIJIGAMBE.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic