Shuti alilopiga kiungo wa Simba, Said Hamis Ndemla dakika ya 14 akimalizia pasi ya Mzamiru Yasin na kumshinda mlinda mlango wa KMC Jonathan Nahima, limekuwa gumzo kubwa.
Simba ilishinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.
Shuti hilo la Ndemla akitumia mguu wa kulia nje ya 18 limekuwa gumzo kubwa mitandaoni.
Ndemla alipiga shuti hilo haraka sana baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mzamiru na kuwaduwaza KMC.
Mjadala huo umekuwa ukiendelea namna shuti hilo alivyoweza kulipiga haraka na kuweza kulenga lango.
Ndemla amekuwa akikaa benchi kutokana na Simba kuwa na kikosi kipana lakini jana alikuwa mmoja wa wachezaji walioonyesha wanaweza kufanya vema wakipata nafasi.
Kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza Saidi kwa mambo kadhaa yaliyonivutia katika mechi ile. Watu watakuwa wanazungumzia bao moja la Saidi Ndemla mimi nimeyaona mabao mawili au matatu muhimu ya Ndemla katika mechi na KMC. (1) Mwili ulioshiba wa mazoezi wenye misuli misili ya tank za gesi. Kwa ghafla sikuweza kumjua ni mchezaji gani tena huyu jamani. Ndemla amekuwa na mwili umebadilika kimazoezi hana tena ule miwili laini wa wachezaji wengi wa kitanzania.(1) Bao kubwa la pili la Ndemla ni ustahamilivu aliouonyesha pale Simba licha ya kupitia kipindi kigumu cha kutokuwa na namba ya uhakika lakini kwakweli Ndemla amekuwa mtulivu katika kipindi chote hicho na cha msingi zaidi amekuwa akijutuma kuinua kiwango chake kuhakikisha anakuwa fiti na kupigania namba kivitendo ushahidi ni kiwamgo alichokionehsa kwa kweli yupo vizuri hata Chama triple " C" ajiangalie zaidi la sivyo chochote kinaweza kutokea kutoka kwa Ndemla.(3) Bao la tatu ni lile shuti alilofumua kufunga lile bao hakika tunahitaji wachezaji wa dizaini ya Saidi Ndemla Tanzania wenye uthubutu wa kufumua mishuti inayolenga goli wanapokaribia kumi nane ya goli. Wachezaji kama Mzamiru, Rashidi Juma wameonesha wanaweza na kama wataongeza bidii basi wale wageni pale Simba wa kazi gani? Jengine viongozi wa Simba wameliona tatizo na kila mtu ameliona tatizo la timu kukata pumzi kipindi cha pili. Vijana wapo vizuri ila wanahitaji mechi zaidi za kujipima nguvu ili kuwa tayari kwa shughuli kama jana. Ifanyike jitihada ya kuwaandalia wachezaji wa akiba mechi nyingi za kirafiki za kimashindano ambazo kuwepo pia na kitu cha kushindiwa katika kila mechi ya kirafiki watakazocheza ili kuitia mechi hiyo ya kirafiki mazingira ya ushindani zaidi.
ReplyDeleteUmenena
Delete