December 30, 2018



Nahodha wa Simba, John Bocco jana alifunga bao katika Ligi Kuu baada ya kupita miezi mitatu ya kupambana kutafuta nafasi ya kufunga bila mafanikio katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa na wakafanikiwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United.

Bocco ana tuzo ya mchezaji bora msimu uliopita na alimaliza akiwa na mabao 14, jana  alifunga bao lake la tatu akimalizia pasi ya Shiza Kichuya dakika ya 17.

Mara ya mwisho Bocco alifunga Septemba 23, mwaka huu katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Katika mchezo huo, Bocco alifunga mabao mawili dakika ya 41 kwa penalti na dakika 45. Bao lingine lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 51. Bao la Mwadui lilifungwa na Charles Ilanfya dakika ya 82ambaye kwa sasa yupo KMC.

Kwa bahati mbaya, katika mchezo huo, Bocco alitolewa uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic