Baada ya jana Azam FC kukubali kupata sare ugenini ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya KMC katika mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru, uongozi wa Azam FC umeelekeza nguvu katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kuwa mpira una matokeo ya aina tofauti hivyo kushindwa kupata ushindi sio mwisho wa mapambano hesabu zake zinasonga mbele.
"Tumeshindwa kupata pointi tatu, sio mbaya kwa kuwa wapinzani wetu walijua wanacheza na timu ya aina gani hali iliyofanya wajitume kupata matokeo, kwa sasa hesabu zetu ni mchezo wetu ujao," alisema.
Azam FC wamefikisha pointi 40 baada ya kucheza michezo 16, Yanga wanashika usukani wa ligi kwa sasa baada ya kucheza michezo 15 wakiwa na pointi 41.
0 COMMENTS:
Post a Comment