December 8, 2018


Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba yule kiungo wao mshambuliaji wa kimataifa aliyetua hapa nchini hivi karibuni akitokea DR Congo, Reuben Bomba, anadaiwa kumalizana na uongozi wa klabu hiyo na ataanza kuitumikia timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Yanga itapambana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wiki ijayo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Ijumaa limezipata zimedai kuwa, Bomba tayari ameshamalizana na Yanga na tayari ameshaanza mazoezi na kikosi cha timu ambacho kitakuwa kikijiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Biashara United ya Mara itakayochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Mechi hiyo Bomba hatacheza.

“Wakati tulipokuwa Mbeya katika mechi yetu na Prisons, Bomba tulimuacha Dar akiwa na viongozi wetu wengine kwa ajili ya mazungumzo naye, wamefika sehemu nzuri.

“Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kuwa tumemalizana naye na kilichobakia ni yeye kusaini tu, lakini mpango uliopo sasa kama mambo yatakuwa sawa basi tunataka mechi dhidi ya Ruvu Shooting aweze kuanza kuitumikia timu yetu,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema: “Kila kitu kuhusiana na Bomba kinaenda vizuri lakini mambo mengine yote yatajulikana hivi karibuni kwani tulikuwa Mbeya na baadaye Rukwa.

“Ila mazungumzo yetu naye yamefikia sehemu nzuri kwa hiyo kila kitu kuhusiana na yaye kitajulikana hivi karibuni.”

5 COMMENTS:

  1. Hujui unachoandika na akili yako inafikiria..Juu halo kwenye kichwa cha habari umeandika biashara..ndani unaandika Ruvu shooting.Saleh Jembe acheni mazoea ya kuandika vichwa visivyoendana na habari ndani.Na kurudia makosa tena na tena ni dalili ya akili finyu..au ujinga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wew utakuwa ndiyo huna akili, na huja soma vizur

      Delete
  2. Mwandishi amesema Yanga na Ruvu Shooting wiki ijayo siyo wiki hii. Sasa kosa lake lipi? Kwan hiyo wiki ijayo si wiki inayoanza 10/12/2018 au hujaelewa? Kesho jumapili Siyo wiki ijayo bado ni wiki hii

    ReplyDelete
  3. Habari ya kwanza kabisha mwandishi aliandika kuanza na Ruvu shooting..Tutazidi kuwakumbusha pale vichwa vya habari visipoendana na habari za ndani mpaka akili zenu za kuandika habari zikomae!Tulishachoka upuuzi na udaku wa saleh jembe

    ReplyDelete
  4. anasema wiki ijayo kwani ITC imesha fika au wanauza gazeti tu me sijaelewa au mchezaji anatembea nayo mfukoni ITC yake magazeti uchwara yanafurahisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic