December 10, 2018


Rais John Magufuli amesema wapo wafanyabiashara wakubwa nchini ambao wamekuwa wakikwepa kodi kwa kupitia makontena wanayoingiza na wengine kupitia njia za mipakani kupeleka biashara zao nje ya nchi.

Magufuli amesema hayo leo wakati akizungumza na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakuu wa Mikoa nchi nzima katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam na kusema majina yao anayo lakini anashangazwa na TRA kutochukua hatua sitahiki.

“Nawataka TPA, TRA, polisi na Idara ya uhamiaji mjirekebishe, vipo vitendo vingi vya kukwamisha wawekezaji naomba mlifanyie kazi. TRA toeni adhabu kwa wakwepa kodi ilimradi msiwaonee na hili litakuwa rahisi tu endapo mtapunguza viwango vya kodi watakuja wenyewe kulipa.

“Wapo watu wamekuwa wakikwepa kodi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tarafa wote mpo. Wakati mwingine naonaga kidogo kwenye TV mmekamata watu, ila najua ile mnafanyajaga kujitangaza kuwa mpo, baada ya muda hali inarudi ile ile.

“Mimi nina majina ya wafanyabiashara wa Kariakoo ambao wanaingiza bidhaa zao bila kulipa kodi kwenye mipaka yetu na wanashirkiana na vyombo vya dola nashangaa wakuu wa wilaya na mikoa hamuwajui. yupo mmoja jina linaishia na ‘AGENCY’, mwingine ‘O’.

“Yupo mfanyabiashara kule Mwanza, halipi kodi na anapitisha magari hata 10 kwa siku moja. Wapo wafanyabiashara wengine wawili wao huleta makontena hadi 700 Kariakoo kwa mwak kisha wanawauzia wengine. Nashangaa TRA, RC Dar hamuwajui.

“Gavana wa BoT (Prof. Florens Luoga) ameeleza hapa alipovamia maduka ya kubadilishia fedha Arusha, alikuta maduka 37 hayana leseni, huku mengine yakifanya biashara bila hata TRA wenyewe kujua na serikali haipati hata shilingi 10.

“Najua kuna kitengo pale TRA mtu akiwa na makosa anafunguliwa kesi baada ya muda kesi inafutwa kwa maelewano maalumu bila huyo mtu kulipa kodi. Wapo wafanyabiashara hutetewa na wanasiasa eti wanasaidia chama, mimi ndiyo mwenyekiti wa chama nasema wote walipe,” amesema Magufuli

1 COMMENTS:

  1. Kodi kwa maendeleo ya nchi ni sawa na matairi na gari angalau likikosa mafuta mnaweza mkalisukuma likasogea lakini sio likikosa matairi litalala tu. Moja ya tatizo kubwa la nchi za kiafrica ikiwemo Tanzania ni kutokuwa na mifumo aminifu na ya uhakika ya ukasanyaji kodi katika vyanzo vyake vya mapato vya ndani na hapo ndipo kwenye kirusi cha umasikini wetu kinapoanzia. Aiza hata kama kutakuwa na mifumo mizuri ya ukasanyaji kodi basi mara nyingi kutakuwepo na ubadhirifu ndani ya maofisa wa kodi katika uchakachuaji wa mapato yanayokusanywa ili kujinufaisha wao wenyewe binafsi. Ni rahisi sana kukusanya kodi kutoka kwa mwananchi wa kawaida kuliko mfanya biashara hasa wafanya biashara wakubwa. Ni rahisi kumuelmisha mwananchi wa kawaida katika kulipa kodi hasa ikiwa kodi anayokatwa inajibu katika kutatua kero zao za msingi kama huduma za maji,barabra na kadhalika. Lakini kwa bahati mbaya kutokana na ubadhirifu uliokuwa ushazoeleka kuwa kama tamaduni ya mtanzania unapoungumzia suala la kodi ya Taifa basi unazungumzia deal la watu fulani fulani hivi na wakati huo huo wananchi wakiichukia kodi na kuona ni uonevu kwao. Kwanza kulikuwa hakuna uwazi hizo pesa zinazokusanywa zinakwenda wapi?kiasi gani kimekusanywa kwa mwezi au mwaka? Kipi hasa kiwango halisi cha ulipaji kodi kwa matabaka mbali ya vyanzo vya makusanyo? Nakadhalika nakadhalika,
    Nchi yoyote duniani inapimwa utukufu wake na usafi katika suala la ufisadi kutokana na jinsi gani watu wake waaminifu katika ulipaji na ukasanyaji wa kodi. Utaona tangu awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikipambana na ufisadi hasa ulipaji wa kodi. Serikali yake imekuwa wazi kabisa kwa wananchi juu ya suala la kodi lakini utaona licha ya jitihada zote hizo lakini bado watu wanaendelea kupiga pengine kisayansi zaidi. Na hii imechangiwa zaidi na ile mizizi ya kifisadi iliyoota kwenye jamii yetu ya kitanzania hasa kwa watendaji wa umma miaka nenda miaka rudi. Kwa kweli muheshimiwa Raisi kajipambanua katika kupambana na masuala mengi ya ufisadi lakini kwa jinsi tunavyoona bado hajapata sapota ya kutosha kutoka katika wakuu wa matawi mengine ya serikali. Kwa mfano taarifa nyingi anazopata muheshimiwa Raisi juu ya vitendo vya ufisadi itakuwa anazipata kutoka kwa vijana wake wa kumletea habari muhimu za siri sasa kwanini wakuu wa mikoa au wilaya washindwe kuwa na watu wao wa siri? wa kujua nani analipa kodi au nani anakwepa kulipa kodi? Kiuhalisia wakuu wa mikoa na wilaya, wao ndio walitakiwa kumjuvya muheshimiwa Raisi juu wakwepaji wa kodi na sio muheshimiwa Raisi kuwajuvya watumishi wake hao kwani wao ndio wapo kwenye field. Kama ni watu wa usalama wa kutafuta habari nyeti wakuu wa mikoa ni wakuu wa ulinzi na usalama katika mikoa yao kwanini wanashindwa kuwa wabunifu kila kitu mpaka wanasubiri kuelekezwa? Kwa kweli kuna tatizo na ni vyema wahusika wakawa watundu wa akili zao kuzituma zaidi ya sasa . Vita hii ya kiuchumi isiwe mzigo wa muheshimiwa Raisi peke yake kwani anaweza kuchoka na asipochoka tunaweza tukamtia maradhi kwani mzee wa watu anaatabika sana kwa ajili ya nchi yetu sote,sapota ni lazima tena ya nguvu kuanza kwa watumishi wa serikali si lazima iwe ya kisiasa lakini ya kimkakati kuhusiana na masuala ya maendeleo ya nchi yetu. Kwa bahati tumepta Raisi aliekuwa gifted kwenye masuala ya Namba hakuna atakaetuibia tukiwa tutaipa serikali yake ushirikiano wa dhati japo kwenda kuripoti ukiona kitendo cha kifisadi kimetokea kuliko kukaa kimya au kununuliwa kwa hadaa iliyojazwa na uchu binafsi. Kwa upande mwengine adhabu zinayotolewa na makosa ya ufisadi zidi ya kodi bado hazina makali ya kutosha kulingana na umuhimu wa kodi na maendeleo ya Taifa kwani kodi ni moja ya Nyara ya muhimu ya Taifa kama si namba moja kwani bila kodi nani atawalipa wanaowahifadhi tembo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic