Zahera alikubali wito wa wachezaji hao ambao wana lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali ya soka ambapo kesho watakuna katika makao makuu ya klabu hiyo.
Taarifa imesema Zahera amekubali kwa moyo mmoja lakini hataki kusikia akigusiwa suala la Kakolanya ambaye alisema hahitaji kumuona tena kwenye kikosi chake.
Kocha huyo mwenye mikwara mizito, amefunguka kuwa anaweza akashindwa kuwasikiliza wachezaji hao wakianza kumzunguzia Kakolanya kwani aligomea mazoezi kisa fedha.
Taarifa imeongeza kuwa Zahera anataka wajadili mambo mbalimbali ikiwemo ya usajili na namna ya kuisaidia Yanga haswa kifedha kutokana na hali inayopitia hivi sasa.








0 COMMENTS:
Post a Comment