December 30, 2018


Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nswanzurimo amesema walishamaliza mchezo wao mapema mbele ya Yanga ila alikwamishwa na uzembe wa mabeki walioshindwa kuwazuia wapinzani wao kufika kwenye eneo la hatari hali pamoja na washambuliaji kukosa umakini.

Katika mchezo wao wa jana dhidi ya Yanga uliochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya City walitengeneza nafasi mbili wakatumia nafasi moja huku Yanga wakitengeneza nafasi mbili na kufunga mabao mawili ambayo yote yalifungwa na Herieter Makambo.

"Mabeki na washambuliaji wangu walishindwa kuwa makini hali iliyofanya tufungwe mabao ya kizembe hasa kipindi cha kwanza, ila ni matokeo na funzo kwetu katika michezo yetu inayofuata tutarekebisha na kufanya vizuri," alisema.

Mbeya City wamecheza michezo 18  ya Ligi wakiwa nafasi ya 9 baada ya kukusanya pointi 23 huku vigogo Yanga wakiendelea kujikita kileleni wakiwa na pointi 50.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic