December 31, 2018


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere ambaye alikosekana kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United kutokana na kusumbuliwa na majeraha, amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na hofu juu yake.

Kagere alipata majeraha hayo katika mchezo wa kimataifa waliocheza dhidi ya Nkana FC ya Zambia amesema kwa sasa anaendelea vizuri hivyo atarejea uwanjani muda wowote akipangwa.

Kagere amesema ushindani ni mkubwa ndani ya Ligi na kila mmoja anatafuta matokeo hivyo wataendelea kupambana kutafuta matokeo.

"Nilishindwa kuanza kucheza dhidi ya Singida United kwa kuwa bado sikuwa fiti kuanza kupambana ila kwa sasa nipo vizuri nipo tayari kwa ajili ya mapambano.

"Mashabiki natambua wanahitaji ushindi ila tumefanikiwa kupata kutokana na wachezaji kucheza kwa kushirikiana, bado kazi inaendelea ili kufikia malengo yetu muhimu sapoti yao," alisema Kagere.

Kutoka Championi

1 COMMENTS:

  1. Ikiwa kama TP Mazembe wanataabika kumnasa Kagere. Kaiser chiefs wanahangaika kumnasa Okwi. Ukiungananisha na wakali wengine Chama, Kotei, Mkude,kichuya,Erasto Nyoni na wakali wengine kadhaa vipi mtu anasubutu kuibeza Simba club bingwa Africa? Kama Simba hii ingekuwa inatoka Kenya tu basi ungeskia jinsi watanzania wanavyoitukuza na kuisifu kwa ubora. Hii tabia ya watanzania kutothamini vya kwao ni dalili tosha yakuwa watanzania bado tunahamu ya kutawaliwa na si ajabu kuona kuna watanzania wamepiga kambi jumuiya ya ulaya na Marekani wakiwashinikkiza wavamizi hao wa kizungu walioivamia Africa miongo michache iliyopita kumdhibiti Magufuli na serikali yake kutoendelea na kuijenga nchi. Mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe
    Waafrica bado hatuja jifunza yaliyotokea Libya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic