December 8, 2018


Wakati dirisha dogo la usajili likiwa bado halijafikia ukingoni, klabu ya Yanga imesema haina mpango wowote wa kuachana na wachezaji wake hivi sasa.

Taarifa ambazo Saleh Jembe imezipata kutoka Idara ya Usajili ndani ya klabu hiyo, zimesema wachezaji wote waliopo wataendelea na majukumu kama kawaida.

Licha ya kupitia wakati wa mpito hivi sasa, timu hiyo itazidi kupigania ubingwa na wachezaji waliopo huku ikiendelea na kusaka wachezaji wengine ili kuziba nyufa kadhaa.

Tayari Yanga inaelekea kukamilisha kumsajili straika mkongomani, Reuben Bomba ambaye ni pendekezo la Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Mkongo huyo yupo hapa nchini na kuna uwezekana akaanza mazoezi siku yoyote kuanzia leo mara baada ya kukamilisha taratibu zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic