December 29, 2018



KIKOSI cha Yanga kimeendeleza ubabe wake leo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wapinzani wao Mbeya City mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga wamefanikiwa kushinda mchezo wa leo kwa idadi ya mabo 2-1 dhidi ya Mbeya City huku mabao yote yakifungwa na Heritier Makambo ambaye kwa sasa anakuwa ni kinara wa mabao akifikisha mabao 11.

Bao la kufuta machozi kwa Mbeya City lilifungwa na Iddy Seleman dakika ya 23 limemfanya kuwa mwiba kila anapokutana na Yanga kwani hata msimu uliopita alipachika bao la kusawazisha dakika za lala salama ila leo wamekubali kupoteza.

Kwa matokeo hayo Yanga wanafikisha mchezo wa 18 bila kupoteza wakiwa wameshinda michezo 16 na kutoa sare michezo miwili kwa mwaka 2018 na kufikisha pointi 50 wakiwaacha mbali Simba kwa jumla ya pointi 20 pamoja na Azam FC kwa poini 10.

14 COMMENTS:

  1. Hawavutii kisoka...ingawa bado wanashinda!

    ReplyDelete
  2. Hivi Yanga alimfunga Singida ngapi walipocheza dar!

    ReplyDelete
  3. Mashujaa walimfunga ngapi cmba walipocheza dar?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mashujaa walicheza na Simba B.Simba A wamefuzu ligi ya Mabingwa..Tungependa kuona itakuwaje Yanga B kama IPO ikicheza na Mashujaa

      Delete
  4. Yanga iliifunga ngapi KMC?Kilikuwa ni kikosi cha pili Yanga?

    ReplyDelete
  5. Yanga ndo Tim pekee yenye uwezo wa kushinda mechi bila wachezaji wake kuwemo

    Mf mechi za mwadui, Africa Lyon, kmc n.k

    Wauweeeeee

    ReplyDelete
    Replies
    1. kumbe bila kuwepo baadhi ya wachezaji na sio Yanga B

      Delete
  6. Kwanini washabiki wa Simba mnakuwa na sababu sababu kila mkifungwa? Mngeshinda dhidi ya Mashujaa mngetangaza ni kikosi B? Kwani kuna nini mkikubali tu kuwa mlizidiwa kisoka na kimbinu na Mashujaa? Wakat mnafungwa na Mbao mlichezesha kikosi gani?

    ReplyDelete
  7. Yanga ameishafungwa na mbao Mara zote wakicheza kirumba..Hawajacheza Kirumba bado..Mwanzoni ilikuwa Ndanda he Ndanda ilifungwa Dar.

    ReplyDelete
  8. Yanga huwa haifungwi .hata mapinduZi cup hawatafungwa..Mwaka Jana ilianza Simba kutolewa na Green Worriers.Yanga haikufuatia?Azam nae keshafungwa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic