KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amefanikiwa kutibua rekodi ya kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC kwa kuwafunga mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Azam FC walikuwa wamecheza michezo 16 ya Ligi Kuu bila kupoteza ila leo katika mchezo wao wa 17 wamekutana na hasira za Mtibwa ambao walitolewa na KCCA katika michuano ya kimataifa.
Katwila amesema walijipanga mapema kutokana na kuwatambua vema wapinzani wao ambao wana kasi ya kushambulia na uwezo wa kubadili matokeo muda wowote uwanjani.
Kwa matokeo hayo Azam FC wanabaki na pointi zao 40 wakiachwa na vinara wa Yanga wenye pointi 50 kwa jumla ya pointi 10 huku wakiendelea kubaki nafasi ya pili na Mtibwa Sugar wakipanda kwa nafasi moja baada ya kufikisha pointi 26 na kuwa nafasi ya nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment