December 31, 2018


Kipa wa Yanga Beno Kakolanya, amesema hawezi kuzungumzia lolote kuhusiana na  Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera juu ya suala lake la kutotakiwa naye kwenye kikosi.

Kakolanya ameeleza kwa sasa jambo hilo lipo nje ya uwezo wake kwakuwa mpaka sasa hajajiunga na kambi ya Yanga.

Kipa huyo ambaye mpaka sasa ana mkataba na Yanga, alikataliwa na Zahera kufuatia kugoma kucheza baada ya malimbikizo ya mshahara kushindwa kupewa.

Kufuatia kitendo hicho, Zahera alikasirishwa na kitendo cha Kakolanya akikichukulia kama utovu wa nidhamu kwakuwa Yanga inapitia wakati mgumu kwa sasa.

Leo Zahera atakutana na wachezaji wa zamani wa Yanga kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya kikosi cha Yanga ikiwemo suala la kuichangia timu.

1 COMMENTS:

  1. Mwandishi wa habari hii ni vyema kuitumia vizuri kalamu yako watu wakuelewe vizuri sio utaje lile jambo la mwisho tu kwa kusema kuwa hatakiwa kambini kwa madai ya kudai malimbikizo ya mshahara tu kabla ya hapo kuna mambo ambayo aliyafanya na hicho ndio kilicho mkera kocha wake sina haja ya kurudia lakini kumbuka huyo mwalimu aliyemkataa Beno asirejee kambini alieleza wazi kisa kizima ambacho kila mtu anakijua na kukielewa vizuri sana ni vyema ukamshauri Beno jambo la kufanya ni kwenda kumuona Kocha wake yeye binafsi na kuongea nae na kumuomba msamaha kama kweli anataka kurejea kwenye timu na wala sio mtu mwengine yeyete ule au njia nengine yeyote ile.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic