KIKOSI cha Yanga kimefanikiwa kuibuka ugenini kwa ushindi wa mabao 2-1 ambayo yamefungwa na Heritier Makambo ambaye kwa sasa anafikisha mabao 11 kwenye orodha ya wafungaji.
Bao la Mbeya City lilifungwa na Iddy Seleman dakika ya 23 kwa kichwa akiwa katikati ya mabeki wa Yanga Kelvin Yondani na Abdalah Shaibu.
Ushindani ni mkubwa kwa kila timu imepambana kutafuta matokeo ambapo Eliud Ambokile wa Mbeya City amewekwa chini ya ulinzi mkali wa Paul Godfrey na Kelvin Yondani ambaye ameonyeshwa kadi ya njano dakika ya 37.
0 COMMENTS:
Post a Comment