December 31, 2018


Kufuatia sakata la kipa Beno Kakolanya na Kocha wake, Mwinyi Zahera kuzidi kushika kasi, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamempa mbinu mchezaji huyo kumalizana kirahisi na Mkongomani huyo.

Mashabiki hao wamemshauri Kakolanya kuacha kujifungia ndani na kukaa kimya na badala yake amfuate Zahera moja kwa moja kumuomba msamaha klabuni.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Zahera kugoma kumsikiliza mtu yoyote anayemtetea Kakolanya kwakuwa aligomea mechi kisa kuidai stahiki zake.

Kuendelea kukosekana kwa Kakolanya ndani ya Yanga kumewafanya baadhi ya mashabiki kuanza kumuonea huruma kipa huyo ambaye alikuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza.

Wengi wamemtaka ni vema akaenda moja kwa moja kwa Zahera mwenyewe aweze kuzungumza naye ili kumaliza suala hilo huku wakiamini atamsahe.

4 COMMENTS:

  1. Sawa kabisa anatakiwa afike mwenyewe kwa Kocha,kocha Kama mzazi ni rahisi kumsamehe badala ya kuwatumia watu wa pembeni

    ReplyDelete
  2. Ni kitu cha kusikitisha sana. Wa kale wamesema: Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe: Kakolanya mpira ndio unaomuendeshea maisha yake ya lazima na ikiwa haki hiyo kwa muda wa miezi kadha amesita kuipata jee anapodai haki hiyo aitwe msaliti na kurakwa yeye akaangukie miguu na siye aliemnyima haki ndio wakumuangukia miguu Kakolinya, hiyo ni sheria ya wapi na jee hao wengine ambao hawajalipwa wataendelea kufanya kazi bila ya kulipwa bila ya kikomo cha kusubiri?

    ReplyDelete
  3. Katika dunia hii kundi la mbuzi wanaopelekwa machungani, wanaochelewesha msafara ni wale mbuzi wambele lakini wanaochapwa ni wale wanyuma

    ReplyDelete
  4. Huyo zahela mpira wa Tanzania hajaujua ipo siku washabiki watamgeuka siku timu ikianza kupoteza mechi hawatamuelewa,au kama vipi na yeye awambie viongozi wa yanga afundishe bure asilipwe mshahara wowote ndo tujue kama kweli anaipenda yanga na ana machungu na timu kakolanya ana haki ya kudai mshahara na si kakolanya tu hata wachezaji wengine wanaodai yanga wanatakiwa walipwe pesa zao kwani ipo siku watachoka kuvumilia na ndo hapo tutaanza kuyaona matokeo uwanjani,kwani wachezaji nao wana watu wanaowategemea na mpira ndio kazi yao,hivyo wito wangu viongozi watafute njia ya kuwalipa wachezaji wote wanaodai mishahara na kocha nae asisimamie msimamo wake ajaribu kumsamehe beno ili kulinda kipaji chake kwani taifa bado linamtegemea,ni maoni tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic