Mashabiki wa Yanga wamemtaka Msemaji wa Simba, Haji Manara kuwaomba radhi wazee wa klabu yao kwa madai mchezaji Cleutus Chama, si hadhi ya Sunday Manara.
Sunday Manara ni baba wa Haji na mchezaji huyo nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, ndiye alikuwa wa kwanza kucheza soka la kulipwa barani Ulaya akitokea Tanzania.
Mashabiki hao wa Yanga waliandika bango lililokuwa likijipambanua namna hii: "Manara waombe radhi wazee wetu, Chama hafikii uwezo wa S. Manara".
`Bango hilo lilionekana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga ikiivaa Biashara kutoka mkoani Mara na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1/
HV huyo chama kafanya jambo gn la maana mpk afananixhwe na Sunday manara(computer)? Huenda hajji manara zmempagawixha hela za no dewji kias cha kuwa mropokaji tu na kukoxa weledi was kaz yke
ReplyDelete