December 19, 2018



Kesho Alhamisi inafanyika droo ya makundi ya michuano ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 ambapo kikosi cha Serengeti Boys ni wenyeji watafahamu wanapangwa na timu gani.

Makundi hayo yanapangwa na msafara wa watu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambao upo nchini kwa ukaguzi kabla ya kufanyika kwa fainali mwakani.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema droo hiyo itafanyika kesho huku timu za mataifa ya Nigeria, Angola, Guinea, Cameroon, Morroco, Senegal, Uganda na wenyeji Tanzania wakisubiri kujua watapangwa kundi gani.

"Droo ya makundi ya Afcon itafanyika kesho Alhamisi na ulimwengu mzima utashuhudia tendo hilo kupitia vyombo vya habari, timu zote zitajua zitapangwa kucheza na nani," alisema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic