Baada ya Yanga kuwashusha kibabe Azam FC kileleni na kuendelea kujikita wakiwa na pointi 44 huku Azam wakiwa na pointi 40, uongozi wa Azam FC umesema kuwa unaitambua dawa itakayowasaidia kurejea kwenye nafasi ya kwanza.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Idd Maganga amesema wanatambua ushindani uliopo ligi Kuu na ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ni lazima wapate matokeo mazuri katika michezo yao.
"Kila baada ya kumaliza mchezo tunatambua kuna kazi mpya inakuja mbele yetu, kama ambavyo ipo kwa sasa, Yanga ni vinara nasi tunafuatia hivyo ili kuweza kurejea kwenye nafasi hiyo ni lazima tupate matokeo.
"Mchezo wetu ujao dhidi ya Mtibwa Sugar tunawaheshimu wapinzani wetu na tutawafuata nyumbani kwao Manungu, Morogoro hesabu zetu ni kupata pointi tatu, wachezaji wameshaanza mazoezi ili kuweza kujijenga," alisema Maganga.
0 COMMENTS:
Post a Comment