December 31, 2018


Licha ya timu ya Yanga kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 50, Nahodha wa zamani wa Simba, Musa Hassan Mgosi amepingana watani zao wa jadi kuchukua ubingwa.

Mgosi ambaye alicheza soka kwa mafanikio Simba, anaamini kikosi cha timu yake kipo vizuri kwa aina ya wachezaji waliopo hivi sasa.

Imani hiyo inamtuma Mgosi kuwa na jeuri ya kuendelea kuutetea ubingwa wa ligi msimu huu licha ya kupoteza mechi moja na kwenda sare mara mbili msimu huu.

"Bado Simba ina nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuangalia aina ya wachezaji ilionao, ni kweli Yanga wanafanya vizuri ila naamini badaye mambo yatakuja kugeuka na tutaendelea kuushikilia ubingwa wetu" alisema.

Katika msimamo wa ligi, Simba imeshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 ikiwa imecheza michezo 14 pekee.





1 COMMENTS:

  1. Labda kama wataendelea kushinda kwa bahati mpaka mwisho! Bahati yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic