HII KALI, MTAYARISHAJI MUZIKI BONGO ATAMANI BIFU LA MONDI NA KIBA LIKOLEE
Kama utani vile lakini ni kweli, unaambiwa mtayarishaji wa ngoma za Bongo Fleva hapa nchini, Man Walter, amesema anatamani kuona bifu la Wasanii Diamond Platnumz na Ali Saleh Kiba likiendelea.
Water ambaye ni mtayarishaji maarufu hapa nchini haswa katika nyimo nyingi za Alikiba, anaamini bifu la wawili hao linaufanya muziki wa Tanzania kuwa na nguvu.
Uwepo wa bifu hilo Water anaamini kabisa linaendeleza muziki wa Tanzania kuwa na ushindani mkubwa kama ilivyo kwa Simba na Yanga.
Mtayarishaji Water ameeleza endapo watakuja kupatana Diamond na Kiba, uwezekano wa muziki wa hapa nyumbani kushuka kiushindani.
Mara ya mwisho Water kuandaa wimbo wa Alikiba ilikuwa ni Mvumo wa Radi ambao ulikuwa maarumu kwa ajili ya kutangaza kinywaji cha Mofaya.








0 COMMENTS:
Post a Comment