December 21, 2018


Uongozi wa timu ya Azam FC umesema kuwa benchi la ufundi lililo chini ya Hans Pluijm linapasua kicwa kufanya vizuri katika michuano ambayo wanashiriki kwa sasa.

Azam FC ambao wapo nafasi ya 2 kwenye Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 40 baada ya kucheza michezo 16, wanashiriki michuano ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na Kombe la Mapinduzi wakiwa ni mabingwa watetezi.

Ofisa habari wa Azam, Jaffary Maganga amesema wanatambua umuhimu wa mashindano wanayoshiriki na wapo tayari kwa ushindani hesabu zao zitaanza kwenye mashindano ya Shirikisho Jumapili watakapocheza na Madini FC.

"Michuano yote kwetu ni muhimu tunaanza na Madini FC kwenye mchezo wetu wa Shirikisho, tutakuwa nyumbani Azam Complex, mchezo utachezwa saa 10:00 na sio saa 1:00 Usiku kama ilivyozoeleka," alisema.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS 
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa. 
Asante 

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic