December 20, 2018

Kikosi cha Yanga kimeendelea kuwa katika ubora wake leo baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Bao pekee lililofungwa na beki Abdalah Shaibu 'Ninja' dakika ya 64 limewafanya waweze kuibuka na pointi tatu muhimu wakiwa ugenini.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga waendelee kujikita kileleni wakiwa na pointi 47 na kuwaacha wapinzani wao Simba wenye pointi 30 kwa pointi 17 wakiwazidi michezo 4 ambayo ni viporo kwa Simba ambao wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga wamefanikiwa kucheza michezo 17 na wameshinda michezo yote bila kupoteza wametoa sare michezo 2 wanafuatiwa na Azam FC nafasi ya pili ambao wanapointi 40 wakiwa wamecheza michezo 16.

2 COMMENTS:

  1. Hii Yanga ni ya pekee!...wako only 15 ambao wanacheza wengine wengi ni majeruhi na wana matatizo mbalimbali lakini waliobaki wanacheza kwa ujasiri, juhudi maelewano na moyo wa kujituma....na hawana first eleven kila mchezaji aliyesajiliwa anatumika!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic