December 21, 2018


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliondoka Dar es Salaam wiki hii na unavyosoma hapa mida hii yupo zake Ufaransa. Lakini yameibuka maneno ya hapa na pale kwamba huenda asirudi.

Lakini yeye amewaambia mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kwamba atarudi, ingawa bado kuna sintofahamu iliyoibuka baina yake na viongozi.

Habari za uhakika kabisa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kwamba Zahera amewaambia watafute tajiri yoyote alipe malimbikizo ya madai ya wachezaji ili kumpunguzia mzigo wa malalamiko, vinginevyo itakuwa ngumu kurejea kwavile anafanya kazi katika mazingira magumu mno.

Kocha huyo ambaye amekwenda kwao ‘kusinya’ (kusaini) mikataba ya leseni za biashara zake, viongozi wamedai ana matatizo ya kesi.

Habari zinasema kwamba, Zahera amewaambia viongozi wa Yanga kwamba kwavile wameshindwa kusainisha wachezaji wapya, akirudi Jangwani Jumatano ijayo anataka akute wamepata chanzo cha fedha cha kulipa wachezaji wote wanaodai na wawe wamelipwa zote au nusu.

Amewaambia kwamba amechoka kuwa msuluhishi wa mambo binafsi ya wachezaji kuhusiana na masilahi kila kukicha badala ya kufanya kazi zake za kiufundi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema kwamba Zahera amechoka na vilio vya fedha za kusaini na mishahara kila kukicha ingawa pedeshee mmoja anayeishi Masaki, Dar es Salaam amemuahidi kwamba wanapambana kuweka mambo sawa.

Kocha amewaambia viongozi ni lazima wawalipe wachezaji wote ambao wanadai fedha zao za usajili na mishahara hata nusu kwa sababu wanaitumikia timu na wanaipambania kwa kila hali.

Amesema kwamba ni lazima wawalipe wachezaji hao kwani kama siyo hivyo yeye hatarudi kuendelea na Yanga kwa sababu amechoka kuwa msuluhishi wa matatizo ya wachezaji,” kilisema chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa Yanga.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili umebaini kwamba, nusu ya kikosi cha Yanga wanadai fedha zao wa usajili lakini kikosi kizima kinadai malimbikizo ya mishahara isiyopungua mitatu.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS 
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa. 
Asante 

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS


CHANZO: SPOTI XTRA

4 COMMENTS:

  1. Nyie Salehjembe Blogspoti ni wachonganishi na wachokozi wa kutaka kuleta vurugu katika timu inayofanya vizuri hebu achaneni na habari za uchonganishi na uchochezi usiokuwa na tija kwa maendeleo ya soka Nani amewaambia kuwa Zahera amesema...hicho chanzo cha habari ni kipi? Hivi kama hakuna habari kwanini msitafute vitu vingine au habari nyingine muendelee kuliuza gazeti lenu? Kuna habari nyingi tu za kuandika...sio hizi za uchonganishi na uzushi uzushi....mnajishushia thamani na weledi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mahsra ya nini ndugu......mbona unateseka?
      Kwa wale majirani zenu simba mbona kupo shwari tu....usione haya nenda kapunguze hasira kule na uwaache waandishi wa habari wafanye kazi yao

      Delete
    2. #Dullyjr Mbona zikiandikwa habari mbaya za simba hua mnapovu kali kupita kawaida mwenzako kacomment unajifanya unajua sana kutetea wandishi wa habari wakati kila siku mnaiponda hii blog haijawai siku kupita hii blog haijapigwa dongo leo imekuaje nzuri kwako kwa vile wameandika issue za upande wa pili?????

      Delete
  2. Sijui lakini, labda mimi naelewa tofauti maana ya hii "CHANZO: SPOTI XTRA". Sioni sababu ya Saleh kulaumiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic