KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema wataimaliza kimyakimya timu ya Azam FC iliyo chini ya kocha Hans Pluijm katika mchezo wao wa Ligi Kuu utakaochezwa uwanja wa Manungu mkoani Morogoro leo.
Mtibwa Sugar watamenyana leo na Azam FC ambao mpaka sasa wamecheza michezo 16 bila kupoteza hata mchezo mmoja kwenye Ligi huku Mtibwa wakiwa wamepoteza michezo 5 kati ya 14 waliyocheza mpaka sasa.
Katwila amesema wanatambua kwamba kikosi cha Azam FC hakijapoteza mchezo mpaka sasa hivyo wao hawana kelele kuwavaa wapinzani hao watawamaliza kimyakimya katika uwanja wao wa nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri.
"Tunawatambua vizuri wapinzani wetu, wamekuja nyumbani kutafuta ushindi ili kulinda rekodi zao basi nasi tumejiaandaa kuwamaliza kibabe na kufanikiwa kuchukua pointi tatu muhimu tukiwa nyumbani.
"Wachezaji nimewajenga kisaikolojia na kuwaambia wasahau yote yaliyopita na sasa kazi ni moja tu kufanya vizuri katika michezo yote tutakayocheza tuweze kujiweka kwenye ushindani zaidi kutafuta ubingwa wa Ligi pamoja na ule wa FA ambao tunaushikilia," alisema Katwila.
Aminiaaa pale mbeya mwingine anyolewe
ReplyDeleteUnaacha kuwaza unatokaje kwa Singida United unawaza yasiyokuhusu kama siyo uchawi ni nini? 😁😁😁😁😁
ReplyDeletemwache akae akitusibiria tupoteze mwakan zikiwa zimebakia mech mbili tuuu
ReplyDelete